728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, July 27, 2015

    SERGIO ROMERO ASAINI MIAKA MITATU MANCHESTER UNITED,DE GEA KAZI ANAYO!!

    U


    Klabu ya Manchester United imeendelea kulitendea haki dirisha la usajili barani Ulaya baada ya kufanikiwa kumnasa bure mlinda mlango Muargentina Sergio Romero.

    Romero,28 ambaye ni mlinda mlango namba moja wa timu ya taifa ya Argentina alikuwa huru baada ya kuachwa na klabu ya Italia ya Sampdoria aliyofanikiwa kuichezea jumla ya michezo kumi tu msimu uliopita.

    Romero amesaini mkataba wa miaka mitatu Manchester United wenye nafasi ya kuongeza mmoja zaidi akichukua nafasi ya mlinda mlango Mhispania Victor Valdes aliyetupiwa virago baada ya kudengua kukichezea kikosi cha timu ya vijana.

    Mbali ya Sampdoria vilabu vingine alivyowahi kuvichezea Sergio Romero ni Az Alkmaar (Uholanzi) na Racing Club (Argentina)

    Van Gaal "Romero ni kijana wangu.Nimefanya nae kazi katika klabu ya Az Alkmaar wakati huo akiwa na miaka 19 tu na tukatwaa ubingwa"

    Romero akiizungumzia Manchester United "Kujiunga na klabu kubwa kama hii ni ndoto iliyotimia.Nasubiri kwa hamu kuanza kuitumikia klabu yangu mpya"
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SERGIO ROMERO ASAINI MIAKA MITATU MANCHESTER UNITED,DE GEA KAZI ANAYO!! Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top