Klabu ya Liverpool imehitimisha ziara yake nchini Australia kwa ushindi wa goli 2-0 dhidi ya klabu ya Adelaide katika mtanange wa kujipima nguvu ulioisha hivi punde.
Liverpool ikicheza katika dimba la Adelaide Oval mbele ya mashabiki 53,0083 ilijipatia magoli yake kupitia kwa nyota wake wapya James Milner na Danny Ings.
Huu ni ushindi wa pili kwa Liverpool baada ya hapo ijumaa usiku kuifunga 2-1 klabu ya Brisbane Roar.
0 comments:
Post a Comment