728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, July 27, 2015

    SIMBA SC BADO YAENDELEA KUKOMAA NA OLUOCH

    Simba bado inaendelea kumtupia jicho kipa wa Gor Mahia, Boniface Oluoch.
    Oluoch ni mmoja wa wachezaji wanaowaniwa na Simba.

    Kipa huyo raia wa Kenya, hivi sasa yupo nchini akiwa na timu yake ya Gor Mahia inayoshiriki michuano ya Kombe la Kagame iliyoanza hivi karibuni.

    Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zakaria Hans Poppe, alisema kuwa uongozi bado unahitaji muda kwa ajili ya kuangalia uwezo wake akiwa golini akiokoa michomo, hivyo wametoa muda wa kumuangalia kipa huyo.

    Hans Poppe alisema, ni ngumu kumpima kipa na kumsajili kwenye mechi mbili au tatu, hivyo wametoa muda zaidi kwa ajili ya kumuangalia kwenye mechi zijazo za Kagame zinazoendelea.

    Aliongeza kuwa, hawana hofu juu ya uwezo wake, lakini kikubwa wanachotaka ni kujiridhisha kipa huyo ana uwezo wa kuidakia Simba na kumpa upinzani Ivo Mapunda pekee.

    “Ni ngumu kumsajili mchezaji kwa kumuangalia kwenye mechi mbili au tatu pekee, kama uongozi tumetoa muda zaidi kwa ajili ya kuuangalia uwezo wa kipa huyo kwenye mechi zijazo za Kagame.
    “Kipa huyo amedaka mechi tatu pekee, ambazo kama uongozi tumetoa muda zaidi wa kumuangalia,” alisema Hans Poppe.

    Kipa huyo hadi hivi sasa amedaka mechi tatu dhidi ya Yanga, Khatoum na KMKM zote amefungwa bao moja moja na kufanya aruhusu mabao matatu pekee.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SIMBA SC BADO YAENDELEA KUKOMAA NA OLUOCH Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top