Klabu ya Arsenal imefanikiwa kutwaa kombe la Emirates baada ya kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya klabu ya Wolfsburg katika mchezo mkali ulioisha hivi punde.
Arsenal ikicheza katika dimba lake la nyumbani la Emirates ilipata goli hilo dakika ya 50 kupitia kwa mshambuliaji wake Theo Walcott aliyeunganisha vyema pasi ya mshambuliaji kinda Jeff Reine-Adelaide.
Ubingwa huu ni wa nne kwa Arsenal tangu michuano hiyo ilipoanza kutimua vumbi lake mwaka 2007 na wa kwanza tangu 2010.
0 comments:
Post a Comment