Sunzu:Mlinzi wa kimataifa wa Zambia Stoppila Sunzu amejiunga na klabu ya Lille ya Ufaransa kwa uhamisho wa mkopo akitokea klabu ya
Shanghai ya China.
Mbemba:Klabu ya Newcastle United imemsajili mlinzi wa Anderletch Chancel Mbemba,20 kwa ada ya £8.5m
Mutu:Mshambuliaji Mromania Adrian Mutu 36 pamoja na kiungo Didier Zokora
34 wamejiunga na klabu ya Fc Pune ya India kwa ajili ya msimu mpya wa
ligi ya nchi hiyo
Gomez:Klabu ya Besiktas ya Uturuki imemsajili kwa mkopo mshambuliaji
Mario Gomez,30 toka klabu ya Fiorentina.Akifanya mahojiano baada ya
uhamisho huo kukamilika Gomez amesema ametua Besiktas ili arejeshe
makali yake na hatimaye arejewe katika kikosi cha timu ya taifa ya
Ujerumani.
Chiriches:Klabu ya Napoli ya Italia imemsajili mlinzi Vlad Chiriches,25
toka klabu ya Tottenham kwa ada ya £4.5m.Chiriches ametua Napoli baada
ya kushindwa kupata namba katika kikosi cha kwanza cha Tottenham
kinachonolewa na Mauricio Pochettino.
Bennacer:Klabu
ya Arsenal imemsajili kinda Mfaransa Ismael Bennacer 18 toka klabu ya
Arles-Avignon kwa ada ya £150,000.Bennacer anacheza nafasi ya kiungo
mshambuliaji.
0 comments:
Post a Comment