728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, July 31, 2015

    FAINALI KAGAME NI AZAM FC NA GOR MAHIA JUMAPILI U/TAIFA



    Klabu ya Azam FC imefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya kombe la Kagame baada ya kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya KCCA ya Uganda katika mchezo mkali uliopigwa jioni ya leo.

    Goli lililoipeleka fainali klabu ya Azam FC limefungwa kipindi cha pili dakika ya 76 na winga wake hatari Farid Mussa akiunganisha krosi ya mshambuliaji Ame Ally "Zungu"

    Katika mchezo mwingine wa nusu fainali uliopigwa majira ya saa 7:30 za mchana Klabu ya FC Gor Mahia ya Kenya iliilaza klabu ya Khartoum N ya Sudan kwa jumla ya goli 3-1.

    Magoli ya Gor Mahia yamefungwa na Michael Olunga kwa mkwaju wa penati,Innocent Wafula na Meddie Kagere huku lile la kufutia machozi la Khartoum likifungwa na Amin Ibrahim Elman.

    Kufuatia matokeo hayo Azam FC na Gor Mahia zitacheza mchezo wa fainali siku ya jumapili ili kumpata bingwa mpya wa michuano ya Kagame na mshindi kuondoka na kikombe pamoja na mamilioni ya dola.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: FAINALI KAGAME NI AZAM FC NA GOR MAHIA JUMAPILI U/TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top