SIMBA ilitaka kushiriki Kombe la Kagame la mwaka huu, lakini
Yanga ikaanzisha chokochoko ikitishia kujitoa kama Mnyama angeingizwa.
Lengo la Jangwani lilikuwa kuhakikisha
inafikia rekodi ya wapinzani wao hao ya kutwaa mara nyingi mataji ya michuano hiyo.
inafikia rekodi ya wapinzani wao hao ya kutwaa mara nyingi mataji ya michuano hiyo.
Simba ndiyo mabingwa wa kihistoria wakiwa
wamenyakua mataji sita tangu michuano hiyo ilipoanzishwa mwaka 1974
wakati Yanga imefanya hivyo mara tano sawa na Gor Mahia, AFC Leopards na
Tusker zote za Kenya.
Hata hivyo hali haikuwa kama ilivyotarajiwa jana
Jumatano kwani mastraika wake nyota; Amissi Tambwe, Donald Ngoma na
Geofrey Mwashiuya walishindwa kufurukuta mbele ya Azam na timu hiyo
kutolewa katika robo fainali kwa mikwaju ya penalti 5-3.
Yanga ilikwama katika pambano hilo lililochezwa
Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza dakika 90 huku
ikibanwa kila kona.
Baada ya mwamuzi, Davies Omweno, kuamuru mikwaju
hiyo ndipo Yanga ikajikuta ikipoteza penalti moja iliyopigwa kidhaifu na
beki wake, Mwinyi Haji.
Azam ilipata penalti zake kupitia Kipre Tchetche,
John Bocco, Himid Mao, Sergie Wawa na Aggrey Morris, huku Salum Telela,
Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Geofrey Mwashiuya wakifunga kwa upande wa
Yanga ambayo haikupiga penalti ya mwisho.
Azam iliyoungwa mkono na mashabiki lukuki wa
Simba, ilionyesha dhamira ya kusonga mbele kwa kuibana Yanga karibu muda
wote wa mchezo.
Mabeki wa kati wa Azam Aggrey Morris na Sergie
Wawa walimdhibiti vilivyo straika mpya wa Yanga, Donald Ngoma kiasi cha
kutokuwa na makeke katika muda wote.
Kwenye penalti Mwinyi alizamisha jahazi la Yanga
kwa mkwaju wake kudakwa na kipa Aishi Manula na safari ya Yanga
kumalizikia hapo.
Kwa ushindi huo Azam itakwaana na KCCA kesho
Ijumaa katika nusu fainali baada ya Waganda hao kushinda mapema jana
mchana dhidi ya Al Shandy kwa mabao 3-0.
Mabao ya KCCA katika mechi hiyo yalitumbukizwa
wavuni na Ochaya Joseph, Matovu Farouq na Tom Masiko. Azam itakutana na
KCCA ikiwa ni mara ya pili, kwani zote zilikuwa kundi moja na katika
mchezo wao Waganda walikubali kipigo cha bao 1-0.
0 comments:
Post a Comment