Wakala wa mlinda mlango wa zamani wa Real Madrid [Iker Casillas] Santon Marguez ameendelea kumshambulia rais wa klabu hiyo Florentino Perez.
Marques ambaye mapema wiki iliyopita alimshutumu Perez kuwa alimuuza kwa nguvu mteja wake [Iker Casilla] kwenda Porto bila ridhaa yake sasa ameibuka na mpya baada ya kudai kuwa rais huyo hapendi wachezaji weusi.
Akifanya mahojiano na kituo cha AS cha Hispania,Marquez amesema "Perez hajaongea ukweli kwa miaka mingi sasa.Anajiona mungu mtu na hakuna anayejua zaidi yake Real Madrid.Watu wanashindwa kumpinga kwa sababu ameshawafanya watumwa.
Alihusika na kuondoka kwa Makelele na Samwel Eto'o.Angalia jinsi alivyoondoka Makelele kwa suala la mshahara tu.Perez siyo mbaguzi lakini hapendi wachezaji weusi.Niligombana naye sana kuhusu Samwel Eto'o.Samwel alikuwa galactico (staa) kama Figo [Luis] lakini aliondoka kutokana na rangi yake ya ngozi.
0 comments:
Post a Comment