Lisbon,Ureno.
KAMPUNI ya kutengeneza vifaa vya michezo ya Nike yenye makao yake makuu nchini Marekani imempongeza balozi wake Mreno,Cristiano Ronaldo kwa mafanikio aliyoyapata msimu huu kwa kumtengenezea viatu vipya aina ya MERCURIAL CAMPEĂ•ES.
Viatu hivyo vya kisasa vimenakishiwa kwa rangi nyekundu ambayo ni rangi ya jezi ya timu ya taifa ya Ureno.Viatu hivyo pia vina nembo ya kibiashara ya Ronaldo ya CR7.Nyuma ya visigino nembo ya timu ya taifa ya Ureno.
Ronaldo ataanza kuonekana akiwa amevaa viatu hivyo hivi karibuni pale atakapokuwa na Ureno kwenye michuano ya kombe la mabara itakayofanyika nchini Urusi.
Kwa mara ya kwanza Ureno itashiriki michuano ya mabara baada ya mwaka jana kutwaa bingwa wa Ulaya kwa kuifunga Ufaransa bao 1-0 kwenye mchezo wa fainali.
0 comments:
Post a Comment