Lyon,Ufaransa.
LYON imeiambia Arsenal kuwa italazimika kukata pochi nene kama kweli inataka kumsajili mshambuliaji wake mahiri,raia wa Ufaransa Alexandre Lacazette.
Kwa mujibu wa gazeti la Telegraph,Lyon inataka ilipwe kitita cha €55m (£48.7m) kama ada ya awali kisha €12m (£10.6m) kama ada ya nyongeza kwa ajili ya mshambuliaji huyo mwenye miaka 26.
Dai hilo limetolewa jana Jumatatu na Rais wa Lyon,Jean-Michael Aulas ambaye mapema wiki iliyopita alifanya kikao na ujumbe wa Arsenal uliofika kumuona ukiongozwa na kocha Arsene Wenger pamoja na Mtendaji Mkuu wa klabu,Ivan Gazidis.
0 comments:
Post a Comment