Dar Es Salaam,Tanzania.
MICHUANO ijayo ya Kombe la SportPesa Super Cup, mwaka 2018,inatarajiwa kufanyika Kenya ikishirikisha timu nane za Kenya na Tanzania.
Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Sport Pesa inayodhamini michuano hiyo, Abbas Tarimba alisema jana
wamefurahishwa na ushindani ulioonyeshwa na timu katika michuano ya mwaka huu iliyomalizika juzi kwa Gor Mahia ya Kenya kutwaa ubingwa huo.
Alisema pamoja na changamoto zilizojitokeza kwenye michuano hiyo,lengo lao la kuzinoa klabu kujiimarisha na ligi zao limefanikiwa na wanafurahi kuona hakuna malalamiko ya timu. “Tunafurahia hamasa na ushindani uliokuwepo kipindi chote cha michuano.
Kwa ujumla mambo yalienda vizuri na tumefanikiwa katika malengo yetu.Ombi langu kwa timu zilizofanya vibaya hasa zaTanzania kujipanga ili mwakani ziweze kufanya vizuri Kenya,” alisema Tarimba.
Kocha Mkuu wa Gor Mahia,
Zedekiah Otieno, alisema siri ya kikosi chake kutwaa taji hilo ni ubora na kutotegemea baadhi ya wachezaji.Otieno alisema walikuja na malengo na kucheza kwa misingi waliyojipangia ndiyo maana
wakafanikiwa kile walichokusudia.
“Nimefurahi kuona tunatwaa
ubingwa huu kwa rekodi ya pekee ya kushinda mechi zote tatu ndani ya muda wa kawaida wa dakika 90.Lakini pia tumecheza bila wachezaji wetu saba ambao wapo kwenye timu zao za taifa. Tunashangaa kuona timu za Tanzania zinasingizia hazikuwa na wachezaji wao
muhimu,” alisema Otieno.
0 comments:
Post a Comment