Dar Es Salaam,Tanzania.
ALIYEKUWA mshambuliaji mahiri na nahodha wa Azam FC,John Bocco 'Adebayor' pichani kulia akikabidhiwa jezi ya Simba SC mara baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia klabu hiyo yenye makao yake makuu mitaa ya Msimbazi,Dar Es Salaam.
Bocco amejiunga na Simba SC baada ya Azam FC kuamua kuachana nae baada ya kuhudumu klabuni hapo kwa kipindi cha zaidi ya miaka kumi.
Bocco anakuwa mchezaji wa tatu kujiunga na Simba SC wiki akitokea Azam FC.Wengine ni mlinda mlango Aishi Manula na mlinzi Shomary Kapombe.Wote wameingia mikataba ya miaka miwili miwili.
0 comments:
Post a Comment