Getafe,Hispania.
TIMU ya CD Tenerife inayochezewa na Mtanzania,Farid Mussa imeshindwa kutinga ligi daraja la kwanza nchini Hispania maarufu kama La Liga baada ya usiku wa kuamkia leo kukubali kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa Getafe katika mchezo mkali wa marudiano uliochezwa kwenye dimba la Uwanja wa Coliseum Alfonso PĂ©rez huko Getafe.
Iliwachukua Getage dakika 8 tu kuandika bao lao la kwanza kupitia kwa Alejandro Faurlin.Dakika ya 12' Dani Pacheco aliifungia Getage bao la pili kabla ya kuongeza tatu katika dakika ya 36.Bao la kufutia machozi la CD Tenerife limefungwa na Tony Lozano katika dakika ya 16.
Hii ina maana Getafe imefanikiwa kupanda La Liga kwa ushindi wa jumla mabao 3-2.Ikumbukwe katika mchezo wa awali uliochezwa Jumatano iliyopita huko Heliodoro,CD Tenerife ilishinda kwa bao 1-0 lililofungwa na Jorge Saenz katika dakika ya 21.
Mara ya mwisho Getafe kupanda La Liga ilikuwa ni msimu wa 2015/16 huku mara ya mwisho kwa CD Tenerife ikiwa ni mwaka 2009 pale iliposhushwa daraja baada ya kuchapwa mabao 3-1 na Valencia katika mchezo wake wa mwisho.
0 comments:
Post a Comment