Riadi,Morocco.
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba SC,Mganda Dan Sserunkuma amejiunga na klabu ya Ittihad Riadi Tanger inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Morocco maarufu kama Botola Pro league.
Sserunkuma amejiunga na Ittihad Riadi Tanger kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Bandari FC ya Kenya aliyoitumikia kwa msimu mmoja akitokea Ulisses FC ya Armenia.Ittihad Riadi Tanger ilishika nafasi ya tano msimu uliopita.
Mshambuliaji huyo mfupi na mwenye umri ulioshiba anakuwa mchezaji wa pili kujiunga na Ittihand Riadi Tanger akiungana na kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast,Lamine Diakite.
Sserunkuma alijiunga na Simba SC Januari 2015 kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Gor Mahia ya Kenya lakini alijikuta akishindwa kuonyesha makali yake Msimbazi na kuamua kuvunja mkataba.
0 comments:
Post a Comment