Harare,Zimbabwe
MSHAMBULIAJI wa Stand United, Abasilim Chidiebele amesaini mkataba wa miaka miwili leo Jumatano kuichezea timu ya Caps United inayoshiriki Ligi Kuu nchini Zimbabwe.
Chidiebele amesaini mkataba huo kwa uhamisho huru baada ya mkataba wake na Stand kumalizika.
Mshambuliaji huyo alisema kuwa usajili wake ulikuwa ufanyike mapema lakini ulichelewa kutokana na kushindwa kufikia makubaliano ya maslahi binafsi ambayo hatimaye wamefikia muafaka baina yake na timu hiyo.
"Napenda kutumia fursa hii
kumshukuru Mungu, familia yangu,Stand United na mashabiki wote wa soka Tanzania kwa kuishi vizuri na mimi katika kipindi chote nilichocheza ligi ya hapo, " alisema mshambuliaji huyo.
0 comments:
Post a Comment