Kazan,Urusi.
TIMU za taifa za Ureno na Mexico zimefanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la mabara baada ya jioni ya leo kushinda michezo yao ya mwisho ya kundi A iliyochezwa kwenye miji ya St Petersburg na Kazan.
Ureno imeitupa nje New Zealand baada ya kuifunga mabao 4-0 katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Krestovskyi uliopo kwenye mji wa St Petersburg.Mabao ya Ureno yamefungwa na Cristiano Ronaldo kwa mkwaju wa penati, Bernardo Silva, Andre Silva na Luis Nani.
Katika mchezo mwingine uliochezwa huko mjini Kazin kwenye Uwanja wa Kazan Arena,Mexico imewatupa nje wenyeji Urusi baada ya kuwafunga mabao 2-1 kwa mabao ya Nestor Araujo na Hirving Lozano.Bao la Urusi limefungwa na Aleksandr Samedov.
0 comments:
Post a Comment