728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, June 24, 2017

    TAIFA STARS DIMBANI KESHO AFRIKA KUSINI


    Rustenburg, Afrika Kusini.

    TIMU ya taifa ya soka ya Tanzania, Taifa Stars inatarajiwa kuanza kutupa karata yake ya kwanza ya kuwania kombe la COSAFA CASTLE kesho Jumapili kwa kuvaana na timu ya taifa ya soka ya Malawi,The Flames.

    Mchezo kati ya Taifa Stars na Malawi utachezwa kwenye Uwanja wa Moruleng mishale ya saa 9:00 za mchana za Afrika Kusini na kufuatiwa na mchezo wa pili kati ya Ushelisheli na Angola utakaochezwa mishale ya saa 11:30 za jioni kwenye Uwanja huohuo.

    Uwanja wa Moruleng ambao hutumiwa na klabu ya Platinum Stars inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Afrika Kusini upo kilometa 60 kutoka kwenye mji wa Rustenburg na una uwezo wa kuchukua watazamaji 20,000.

    Tanzania imepangwa kundi A pamoja na timu za taifa za Malawi,Ushelisheli pamoja na Angola.Mshindi wa kwanza wa kundi A atafuzu robo fainali na kucheza na wenyeji Afrika Kusini ambao pia ni mabingwa watetezi wa michuano hiyo.

    Tanzania imealikwa kushiriki michuano ya COSAFA ya mwaka huu kuchukua nafasi ya Comoro iliyojitoa katika dakika za mwisho kwa sababu ambazo hazijawekwa wazi.

    Michuano ya kombe la COSAFA CASTLE imepangwa kuanza kutimua vumbi lake Juni 25 na kuishia Julai 9 ambapo jumla ya timu 14 zitachuana kumsaka mshindi mmoja.

    Michuano ya COSAFA huandaliwa kila mwaka na baraza la mpira wa miguu la nchi za kusini mwa Afrika (COSAFA) kwa kushirikiana na kampuni ya kutengeneza vinyaji vikali ya Afrika Kusini ya Castle Lager.

    Kikosi cha Taifa Stars ambacho kitashiriki michuano ya COSAFA CASTLE ni makipa Aishi Salum Manula (Azam FC),Benno David Kakolanya (Young Africans SC) na Said Mohammed Said
    (Mtibwa Sugar FC).

    Mabeki ni Shomari Salum Kapombe (Azam FC) na Hassan Hamis Ramadhan
    ‘Kessy’ (Young Africans ) Gadiel Michael (Azam FC),Hamim Abdulkarim (Toto
    Africans FC).

    Erasto Nyoni (Azam FC), Salim Hassan Abdallah (Mtibwa Sugar), Abdi Hassan Banda (Simba SC) na Nurdin Chona (Tanzania Prisons).

    Viungo ni Himid Mao Mkami (Azam FC) na Salmin Hoza wa Mbao FC,Mzamiru Yassin Selembe (Simba), Simon Happygod Msuva (Young Africans SC), Raphael Daudi (Mbeya City) na Shizza Ramadhani Kichuya (Simba SC).

    Washambuliaji ni Thomas Emmanuel Ulimwengu (AFC Eskilstuna-Sweden), Mbaraka Abeid Yusufu (Kagera Sugar),
    Stamili Mbonde, Elius Maguli (Dhofar SC) na Shabani Idd Chilunda (Azam FC).

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: TAIFA STARS DIMBANI KESHO AFRIKA KUSINI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top