728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, September 05, 2016

    VPL:YANGA SC YAIFUATA NDANDA FC BILA YA NYOTA WAKE SITA

    Dar Es Salaam,Tanzania.

    MSAFARA wa mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara,Yanga SC,unatarajiwa kuondoka jijini Dar Es Salaam, Jumanne Alfajiri ukiwa na kikosi cha nyota 20 na jopo la ufundi lenye watu 7 likiongozwa na Kocha Hans Van Pluijm  kuelekea mkoani Mtwara tayari kwa ajili ya mchezo wao wa kesho kutwa Jumatano dhidi ya wenyeji wao Ndanda FC.

    Katika mchezo huo unaotarajiwa kuwa na vuta nikuvute nyingi Yanga SC itawakosa nyota wake sita kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ugonjwa na majukumu ya timu za taifa.

    Nyota wataokaoukosa mchezo huo ambao ni wa pili kwa Yanga SC ni:

    1. Deogratius Munishi ( Msibani )
    2. Geofrey Mwashuiya ( majerhi )
    3. Pato Ngonyani ( majeruhi )
    4. Malimi Busungu ( majeruhi )
    5. Haruna Niyonzima ( timu ya taifa )
    6. Vicenti Bossou ( timu ya taifa )


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: VPL:YANGA SC YAIFUATA NDANDA FC BILA YA NYOTA WAKE SITA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top