Toulouse,Ufaransa.
HISPANIA imeanza vyema kuutetea ubingwa wake wa Ulaya baada ya jioni ya leo kuichapa Czech kwa bao 1-0 katika mchezo mkali wa Kundi D uliochezwa katika uwanja wa Stadium de Toulouse ulioko jijini Toulouse.
Bao pekee la mchezo huo limefungwa dakika ya 87 na mlinzi Gerrard Pique akiunganisha krosi safi ya Andres Iniesta.
0 comments:
Post a Comment