728x90 AdSpace

Sunday, June 26, 2016

MASUMBWI:ANTONY JOSHUA AENDELEZA UBABE KWA MABONDIA WA MAREKANI AMCHAPA DOMINIC BREAZEALE KWA KO

London,England.

BONDIA wa Uingereza Anthony Joshua,26, ameendeleza ubabe kwa mabondia wa Marekani baada ya Usiku huu kumchapa Dominic Breazeale,30, kwa Knockout ya Raundi ya saba na Kufanikiwa kuutetea ubingwa wake wa dunia wa IBF katika pambano kali lililofanyika katika ukumbi wa O2 Arena,jijini London- England.

Mwamuzi Howard Foster alilazimika kulimaliza pambano Raundi ya saba baada ya Breazeale kushindwa kuamka baada ya kuchapwa konde Kali na Joshua.Kwa ushindi huo Joshua amefanikiwa kushinda michezo 17 kwa KO kati ya michezo 17 aliyocheza.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: MASUMBWI:ANTONY JOSHUA AENDELEZA UBABE KWA MABONDIA WA MAREKANI AMCHAPA DOMINIC BREAZEALE KWA KO Rating: 5 Reviewed By: Unknown