728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, June 21, 2016

    EURO 2016:WALES KIDEDEA KUNDI B,ENGLAND YA PILI,SLOVAKIA KUINGIA KWA MLANGO WA NYUMA

    Toulouse,Ufaransa.

    WALES imefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora ya michuano ya Ulaya/Ulaya ikiwa kinara wa Kundi B baada ya usiku wa leo kuifumua Urusi kwa mabao 3-0 katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi uliochezwa katika uwanja wa Stade de Toulouse (Municipal) na kushuhudiwa na watazamaji 28840.

    Mabao yaliyoipa Wales ushindi huo wa Kihistoria yamefungwa na Aaron Ramsey dakika ya 11,Neil Taylor dakika ya 20 na Gareth Bale dakika ya 67.

    Katika mchezo wa pili uliochezwa huko Nice katika uwanja wa Geoffroy-Guichard mbele ya watazamani 30,531,England nayo imefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora ya michuano hiyo licha ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na Slovakia.

    Kwa matokeo hayo Wales imefanikiwa kuongoza kundi B ikiwa na pointi sita,nafasi ya pili imeshikwa na England yenye pointi tano,Slovakia ni ya tatu ikiwa na pointi zake nne na inaweza kutinga 16 bora kutokana na kuwa na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.


    Katika hatua ya 16 bora England huenda ikavaana na Ureno ama Iceland,Wales wao watavaana na mshindi wa tatu toka kati ya makundi A,C ama D ambaye yaweza kuwa Albania,Jamhuri ya Ireland,Czech,Poland au Croatia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: EURO 2016:WALES KIDEDEA KUNDI B,ENGLAND YA PILI,SLOVAKIA KUINGIA KWA MLANGO WA NYUMA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top