Dar es Salaam,Tanzania.
MSHAMBULIAJI Mtanzania anayecheza katika klabu ya TP Mazembe ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Thomas Ulimwengu, amesema
kiwango kilichoonyeshwa na Mzambia, Obrey Chirwa wa Yanga ni cha
kawaida sana.
Chirwa amesajiliwa Yanga katika kipindi cha dirisha dogo la usajili
katika michuano ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) akitokea Platnum ya
Zimbabwe.
Mchezaji huyo alikuwa katika kikosi cha Yanga kilichocheza juzi na TP
Mazembe kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambao walifungwa
bao 1-0.
Akimzungumzia Chirwa, Ulimwengu alisema kiwango kilichoonyesha na
mchezaji huyo ni cha kawaida na anatakiwa kupewa muda ili aweze
kuonyesha uwezo wake.
Ulimwengu alisema Chirwa anahitaji muda kwani anaonekana hajawa fiti kucheza soka la Tanzania.
“Chirwa anaonekana mgeni, halijui soka la Tanzania wala viwanja vyake
tofauti na Mahadhi ambaye Uwanja wa Taifa si mara ya kwanza kucheza,”
alisema Ulimwengu.
Ulimwengu alisema mchezaji huyo si mbaya, lakini anaonekana bado
mgeni kutokana na mazingira ila akiendelea kucheza anaweza kuwa tishio.
CHANZO:BINGWA
0 comments:
Post a Comment