728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, June 22, 2016

    AZAM FC YATANGAZA KUACHANA NA KIPA IVO MAPUNDA

    Dar es Salaam,Tanzania.

    MABINGWA wa Soka wa Afrika Mashariki na Kati,Azam FC wametangaza kumtema kipa wao Mkongwe, Ivo Mapunda kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kushindwa kuridhishwa na kiwango chake tangu alipotua klabuni hapo msimu mmoja uliopita akitokea Simba SC.

    Azam FC ilimsajili Ivo,34,msimu uliopita akiwa mchezaji huru baada ya iliyokuwa klabu yake ya Simba SC kugoma kumpa mkataba mpya kufuatia ule wa awali kuwa umekwisha.

    Tangu atue Azam FC, Ivo ameshindwa kupata namba kikosi cha kwanza kutokana na kujikuta akiwa kipa chaguo la tatu nyuma ya Aishi Manula na Mwadini A. Mwadini hali iliyofanya klabu isite kumpa mkataba mpya na kuamua kutafuta kipa mwingine.

    Akidhibitisha habari hizo Katibu Mkuu wa Azam FC, Idrisa Nassor amesema kuwa, Klabu yake haitaendelea na Ivo katika msimu ujao wa Ligi Kuu na kwa sasa wanafanya mchakato wa kusajili kipa mwingine atakayeziba nafasi yake.

    “Kwasasa Ivo amebakiza miezi mitatu ili kukamilisha mkataba wake na Azam FC
    aliousaini msimu uliopita na baada ya hapo tutaagana. 


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: AZAM FC YATANGAZA KUACHANA NA KIPA IVO MAPUNDA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top