728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, June 26, 2016

    PLUIJM AFUNGA USAJILI YANGA SC

    Dar es Salaam,Tanzania.

    KOCHA wa Yanga, Hans Pluijm amesema hatarajii kusajili mchezaji mwingine mpya kutoka ndani au nje
    ya Tanzania baada ya kuinasa saini ya mshambuliaji raia wa Zambia Obrey Chirwa.

    Dirisha la usajili tayari limefunguliwa tangu Juni 15, na Yanga imekamilisha usajili wake wa msimu ujao kwa kuwanyakua Hassan Ramadhani ‘Kessy’, Juma Mahadhi,Andrew Vicent ‘Dante’, Beno Kakolanya na Chirwa.

    Pluijm, amesema anaridhishwa na viwango vya wachezaji aliowasajili
    na sasa kikosi chake kimetimia kwa kuziba upungufu uliokuwepo.

    “Tulikuwa na mapungufu madogo msimu uliopita katika baadhi ya nafasi, nafurahi kuona hadi kufikia sasa tumeshayaziba na kikosi kimekamilika kwa ajili ya mapambano ya michuano tunayoshiriki,” alisema Pluijm.

    Kocha huyo raia wa Uholanzi,alisema hakupenda kusajili kundi kubwa la wachezaji wapya, kwani kungewachukua muda mrefu kwa ajili ya kuzoeana na wenzao na mfumo anaoutumia, kitu ambacho kingechangia kuanza vibaya msimu ujao au hata kushindwa kupata mafanikio.

    Alisema mafanikio yao ya msimu uliopita yalitokana na wachezaji wengi wa kikosi chake kukaa kwa muda mrefu na kuzoeana na hata wachezaji wachache aliowasajili walikuwa na uwezo mkubwa ambao haikuwa tabu kuwaunganisha na waliokuwepo.

    “Bado tunayo nafasi ya kufanya usajili, lakini kwa sasa nina imani na wachezaji waliopo, tunaweza kufanya hivyo, labda kama ikitokea kupata majeruhi wa muda,vinginevyo timu yangu ipo imara kwa ajili ya mashindano yote tutakayoshiriki,” alisema Pluijm.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: PLUIJM AFUNGA USAJILI YANGA SC Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top