Chicago,Marekani.
MABINGWA watetezi CHILE wametinga Fainali ya pili mfululizo ya michuano ya Copa America Centenario baada ya Alfajiri ya leo kuichapa Colombia kwa mabao 2-0 katika mchezo mkali wa nusu fainali uliochezwa katika uwanja wa Jeshi (Soldier Field) huko Chicago,Marekani.
Katika mchezo uliosimama kwa muda mrefu kupisha mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha ilishuhudiwa Chile ikipata mabao yake ya ushindi ndani ya dakika 11 za kipindi cha kwanza kupitia kwa Charles Aranguiz na Jose Fuenzalida.
Kwa matokeo hayo Chile itavaana na Argentina katika mchezo wa Fainali utakaochezwa siku ya Jumapili Juni 26 katika uwanja wa MetLife Stadium huko East Rutherford, New Jersey.
Fainali hii ni kama marudio kwani Chile na Argentina zilikutana katika mchezo wa Fainali mwaka jana na Chile kuibuka mabingwa baada ya kuifunga Argentina kwa changamoto ya mikwaju ya penati.
0 comments:
Post a Comment