Houston,Marekani.
ARGENTINA imetinga Fainali ya Michuano ya Copa America Centenario baada Alfajiri ya leo kuwafunga wenyeji wa Michuano hiyo Marekani kwa mabao 4-0 katika Mchezo wa Nusu Fainali uliochezwa katika uwanja wa NRG Stadium, Houston, Texas.
Mabao ya Argentina yamefungwa na Ezequel Lavezzi 3',Lionel Messi 32' kwa mkwaju wa Faulo na Gonzalo Higuain 50' na 85'.
Katika mchezo huo Lionel Messi amechagulia kuwa mchezaji bora wa Mechi baada ya kufunga bao moja na kutengeneza mengine mawili.Pia bao hilo moja limemfanya Messi afikishe mabao 55 na kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Argentina hii ni baada ya kuivuka rekodi ya mabao 54 ya nyota wa zamani wa timu hiyo Gabriel Batistuta.
VIKOSI
United States
XI: Guzan; Yedlin, Cameron, Brooks,Johnson; Zusi, Beckerman, Bradley,Zardes; Dempsey, Wondolowski
Argentina
XI: Romero; Mercado, Otamendi, Funes
Mori,Rojo;Augusto,Mascherano,Banega; Messi, Higuain, Lavezzi
Nusu Fainali itachezwa hapo Kesho Alhamis ambapo Mabingwa watetezi Chile watavaana na Colombia na mashindi atafuzu Fainali kucheza na Argentina inayopambana kutwaa taji kubwa la Kwanza baada ya ukame wa miaka 23.
Safiiii
ReplyDelete