Romelu Lukaku
Lukaku:Mwandishi wa habari za Michezo, Muitalia Emanuele Giulianelli ameripoti kuwa mshambuliaji wa Everton, Romelu Lukaku,23,hatajiunga na Chelsea na badala yake atatimkia Arsenal hii ni baada ya kukubaliana maslahi binafsi na miamba hiyo ya Emirates.(Team Talk)
Vardy:Baada ya Jamie Jardy,29, kuamua kuitosa Arsenal na kubaki Leceister City habari kutoka England zinasema staa huyo wa zamani wa Freetwood Town ameamua kubadilisha mawazo baada ya kuhisi kuwa aina yake ya uchezaji ni tofauti sana na ile ya Arsenal ya pasi nyingi hivyo ingemuwia ugumu kutamba Emirates.(Sky Sport)
Tchetche:Azam FC imesema iko tayari kumuuza mshambuliaji wake Kipre Tchetche kwenda kokote kule ilimradi tu timu inayomtaka staa huyo wa Ivory Coast ifuate taratibu stahiki badala ya kutumia njia za panya.(Saleh Jembe)
Christensen:Chelsea imekataa dau la £18m kutoka Borussia Monchengladbach kwa ajili ya kumuuza beki wake,Andreas Christensen.
(Mail )
Lacazette:West Ham United imepania kumsajili Mshambuliaji Mfaransa,Alexandre Lacazette, 25, hii ni baada ya kutuma ofa ya €52m (£41.6m) kwenda katika klabu yake ya Lyon.(L'Equipe )
Blanc:Meneja Laurent Blanc amelipwa kitita cha €22m kama fidia baada ya Paris Saint Germain kuamua kuachana nae.(L'Equipe)
Mangala:FC Porto inataka kumsajili kwa mkopo wa mwaka mmoja beki wake wa zamani ambaye kwasasa yuko Manchester City,Eliaquim Mangala,25, na kisha kumsajili moja kwa moja hapo baadae.( O Jogo)
Slimani:Arsenal inajaribu kupoza machungu ya kutoswa na Jamie Vardy kwa kuendelea na msako wa mshambuliaji mpya na safari hii imeripotiwa kuelekeza nguvu zake kwa mshambuliaji wa Sporting Lisbon,Mualgeria, Islam Slimani. Msimu uliopita Slimani,24,aliifungia Sporting Lisbon mabao 31 katika michezo 46.Slimani anapatikana kwa dau la €30m.(A Bola)
Carrasco:Arsenal imedaiwa kuwa itamgeukia winga wa Atletico Madrid,Yannick Carrasco ikiwa itashindwa jaribio lake la kutaka kumsajili staa wa Borussia Dortmund,Henrikh
Mkhitaryan,27.(Emanuele Giulianelli)
Benteke:Meneja wa Crystal Palace,Alan Pardew anataka kukiimarisha kikosi chake kwa kumsajili mshambuliaji wa Liverpool, Christian Benteke,24.(The Sun)
Adam:Burnely ambayo imepanda daraja msimu huu inataka kuvamia katika vilabu vya Stoke City na Crystal Palace na kuwasajili kiungo Charlie Adam na beki Joe Ledley (Daily
Star/ The Sun)
Robertson:Liverpool italazimika kutoa £12m ili kuweza kuipata saini ya beki wa Hull City,Mscotland, Andy Robertson.(Daily Mirror)
Valencia:West Ham United imepanga kuachana na mshambuliaji wake ,Enner Valencia ,hii ni baada ya kutangaza kuwa itamuuza kwa dau la £7.5m.(Cronuca)
0 comments:
Post a Comment