728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, June 27, 2016

    BAADA YA TAMBWE,NGOMA KUZICHAPA KAVUKAVU YADAIWA HIKI NDICHO CHANZO CHA UGOMVI WAO


    Dar es Salaam,Tanzania.

    WAKATI wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika wakiwa kwenye maandalizi ya mwisho ya mchezo wao wa pili hatua ya makundi dhidi ya TP Mazembe ya Congo, inadaiwa kuwa mastarika wake wa kimataifa, Amissi Tambwe (Burundi) na Donald Ngoma (Zimbabwe), wametofautiana na kusababisha wawili hao kuzichapa kavukavu.

    Tukio hilo linaloonekana huenda likajenga uhasama baina ya wachezaji hao, lilitokea Ijumaa iliyopita wakati wakiwa kwenye mazoezi ya mwisho nchini Uturuki walikokuwa wameweka kambi ya wiki mbili kabla ya kurejea nyumbani kuwavaa TP Mazembe hapo kesho.

    Kwa mujibu wa mmoja wa mashuhuda ni kuwa jambo hilo lilitokea baada ya Ngoma kufunga bao lililoonekana ni la kuotea na kocha Hans Van Pluijm kutopiga filimbi kuashiria kuwa bao hilo ni la kuotea wakati awali Tambwe alifunga bao kama hilo na kocha alipiga filimbi kuashiria Mrundi huyo aliotea.

    “Hakuna mtu ambaye aliwaza kama wawili hao wangeweza kukunjana na hatimaye kupigana. Ilikuwa kama kawaida ya kocha aliweka timu A na B, wakati wakiendelea kucheza golini akiwa Ally Mustapha ‘Barthez’ , Tambwe alifunga bao ambalo kocha lilikataa akidai lilikuwa la kuotea na muda mfupi, Ngoma naye akafunga kama lile la kwanza lakini kocha hakupiga filimbi.

    “Ndipo Tambwe na wachezaji wengine
    walipomweleza Ngoma kuwa halikuwa bao halali, cha ajabu Ngoma alimfuata Tambwe na kumwambia kwanini aseme hivyo wakati hata yeye anapendelewa na kocha mara nyingi, lakini pia Ngoma alimweleza Tambwe kuwa muda wake wa kukaa benchi umefika
    kwani mchezaji mpya Mzambia, Obrey Chirwa ni mzuri zaidi yake,” alisema mtoa habari huyo na kuongeza:

    “Baada ya kuambiwa hivyo, Tambwe alimjibu Ngoma kuwa kila mmoja ataonyesha uwezo wake uwanjani, lakini ghafla Ngoma akamvaa Tambwe na kuanza kumshushia kipigo jambo lililowalazimu wachezaji na viongozi kuingilia kati suala hilo kipindi ambacho tayari Tambwe alishaumia.”

    Mtoa habari huyo aliongeza kuwa ilimlazimu daktari kumpa huduma ya kwanza Tambwe na baadaye akapelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu zaidi huku baadhi ya wachezaji sita akiwemo Ngoma wakirejea Jumamosi huku Tambwe akirejea Tanzania jana.


    CHANZO:BINGWA


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BAADA YA TAMBWE,NGOMA KUZICHAPA KAVUKAVU YADAIWA HIKI NDICHO CHANZO CHA UGOMVI WAO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top