Lyon,Ufaransa.
MABAO mawili ya Cristiano Ronaldo na moja la Luis Nani yameipa Ureno sare ya mabao 3-3 na Hungary katika mchezo wa kundi F uliochezwa katika uwanja wa Estadio de Lumieres.
Mabao ya Hungary yamefungwa na Zoltan Gera na Balazs Dzsudzsak aliyefunga mabao mawili.
Kwa matokeo hayo Hungary imefuzu hatua ya 16 bora baada ya kumaliza kileleni mwa Kundi F ikiwa na alama tano sawa na Iceland,Ureno nayo pia imefuzu licha ya kumaliza katika nafasi ya tatu ikiwa na alama tatu.
Katika hatu ya 16 bora Ureno itavaana na Croatia huku Iceland ikivaana na England
VIKOSI
Hungary: Kiraly, Lang, Juhasz, Guzmics,
Korhut, Pinter, Elek, Lovrencsics, Gera,
Dzsudzsak, Szalai.
Portugal: Patricio, Vieirinha, Pepe, R Carvalho, Eliseu, Gomes, W Carvalho,Moutinho, Nani, Ronaldo,Joao.
0 comments:
Post a Comment