Nice,Ufaransa.
ENGLAND imetupwa nje ya michuano ya Euro 2016 baada ya usiku huu kuchapwa mabao 2-1 na Iceland katika mchezo wa mtoano uliochezwa katika uwanja wa Stade de Riviera,Nice.
Wayne Rooney alianza kuifungia England bao la kuongoza kwa mkwaju wa penati kabla ya Iceland kusawazisha kupitia kwa Ragnar Sigurdsson na kisha kupata bao la ushindi kupitia kwa Kolbeinn Sigthorsson
Wakati huohuo Kocha wa England,Roy Hodgson ametangaza kubwaga manyanga kuifundisha timu mara tu baada ya kuishuhudia timu yake ikiaga michuano ya Euro 2016.
Mbali ya Hodgson wasaidizi wake Ray Lewington na Gary Neville nao wanatarajiwa kujiondoa ili kutoa nafasi kwa chama cha soka cha England (FA) kusaka benchi jipya la ufundi.
Iceland itacheza Robo Fainali kwa kuvaana na wenyeji Ufaransa.
0 comments:
Post a Comment