Mchezaji bora wa Copa America:Alexis Sánchez
New Jersey,Marekani.
SHIRIKISHO la Soka la Amerika Kusini CONMEBOL limetoa majina ya wachezaji XI waliofanya vizuri katika michuano ya Copa America Centenario iliyofikia tamati yake Alfajiri ya jana Jumatatu na Chile kuibuka Mabingwa kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuwafunga Argentina kwa penati 4-2 katika mchezo mkali wa Finali uliochezwa katika uwanja wa MetLife huko New Jersey,Marekani.
Katika kikosi hicho Mabingwa Chile wameingiza wachezaji wanane ambao ni Claudio Bravo,Mauricio Isla, Gary Medel na Jean Beausejour.
Wengine ni Arturo Vidal,Charles Aranguiz,Alexis Sánchez na Eduardo Vargas.
Argentina wao wameingiza wachezaji watatu ambao ni Nicolás Otamendi ,Javier Mascherano na Lionel Messi.
0 comments:
Post a Comment