Liverpool, England.
KUNA kila dalili kuwa Sadio Mane atakuwa mchezaji mpya wa Liverpool ndani ya kipindi kifupi kijacho hii ni baada ya klabu yake ya Southampton kukubali ofa ya £30m toka kwa miamba hiyo ya Merseyside.
Southampton imekubali kumuuza Mane,24,kwenda Liverpool baada ya siku ya Ijumaa kumsajili Nathan Redmond kutoka Norwich City kwa ada ya uhamisho ya £11m.
Mane anatarajiwa kuwasili leo Jumatatu yalipo makao makuu ya Liverpool huko Merseyside kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya na ikiwa atafaulu atasaini kandarasi ya miaka mitano ya kuwatumikia mabingwa hao wa zamani wa Ulaya.
Ikiwa kila kitu kitakwenda sawa,basi Mane atakuwa mchezaji wa tano toka Southampton kujiunga na Liverpool katika kipindi kisichozidi miaka mitatu.
Wengine ni Rickie Lambert, Adam Lallana, Dejan Lovren na Nathaniel Clyne na kuifanya Southampton iwe imejipatia faida ya £92m katika mauzo ya wachezaji hao.
Mpaka sasa Liverpool imeshawanasa wachezaji watatu ambao ni Marko Grujic, Joel Matip na Loris Karius tayari kwa msimu mpya wa 2016/17.
0 comments:
Post a Comment