Marseille,Ufaransa.
KATIKA hali isiyotarajiwa na wengi Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Ubelgiji,Marc Wilmots amemruhusu Kiungo wake, Radja Nainggolan kuvuta sigara awezavyo lakini ahakikishe kuwa anafanya vizuri Uwanjani.
Hatua hiyo ya Wilmots ni kinyume na misimamo ya Makocha wengi ambao wamekuwa hawataki kufanya kazi ama kuwa na wachezaji ambao wanavuta sigara katika vikosi vyao.
Akiongeza na Sporza.be, Wilmots amekiri nyota huyo wa AS Roma kubobea katika uvutaji wa sigara na kusisitiza kuwa amemuandalia mazingira mazuri ya kuvutia sigara zake ili asijione kuwa anabanwa.
Amesema “Ni kweli Radja ni mvutaji mzuri wa sigara na ni mchezaji pekee mwenye tabia hiyo katika kikosi changu.Nimempa ruhusa avute."
Wilmots ameongeza “Ni tabia ambayo iko Ufaransa na Italia,ambapo wachezaji wengi wanavuta sigara.Simzuii kuvuta sigara.Ni mwili wake lakini kama anavuta na anaendelea kuonyesha kiwango kizuri,sina tatizo nae kabisa.
Lakini kama atajikuta anastaafu mpira akiwa na miaka 30 badala ya 35 hilo litakuwa ni tatizo lake na siyo langu".
0 comments:
Post a Comment