Youssef Aït Bennasser
Maguli:Mshambuliaji wa Stand United,Elius Maguli ameiacha kwenye mataa Klabu ya Super Sport ya Afrika Kusini iliyokuwa inamuhitaji kwa ajili ya kumfanyia majaribio na badala yake ametimkia nchini Oman kujaribu bahati yake katika klabu ambayo bado haijawekwa wazi.(Binzubery)
Lukaku:Everton imeanza mipango ya kuhakikisha mshambuliaji wake, Romelu Lukaku anasalia klabuni hapo msimu ujao hii ni baada ya Mmiliki mpya wa Klabu hiyo Farhad Moshiri kujiandaa kumpa kandarasi mpya mkali huyo ya mabao. Kandarasi hiyo mpya itakayokuwa ya miaka mitano itamuwezesha Lukaku,23,kuvuna mshahara ya £100,000 kwa wiki.(Daily Telegraph)
Pjaca:Liverpool imeripotiwa kuendelea na mipango ya kukiongeza nguvu kikosi chake hii ni baada ya kutajwa kuwa ni miongoni vilabu vinavyomtaka winga wa Croatia na Dinamo Zagreb ,Marko Pjaca,21,mwenye thamani ya £12m.(Gazzetta dello Sport)
Bellarabi:Borussia Dortmund imeanza kujiandaa na maisha bila ya kiungo wake, Henrikh Mkhitaryan baada ya kuripotiwa kuanza kumfukuzia kiungo wa Bayer Leverkusen, Karim Bellarabi.Msimu uliopita Bellarabi,26,aliifungia Bayer Leverkusen mabao 12 katika michezo 40.(Bild)
Grosicki:Meneja wa Everton, Ronald Koeman anataka kufanya usajili wa pili tangu atue Goodson Park kwa kumsajili winga wa Rennes na Poland, Kamil Grosicki,25.(Le Telegramme)
Tore:West Ham United imefikia hatua nzuri katika mbio zake za kumuwania winga wa Besiktas, Gökhan Tore baada ya ofa yake ya €13m kukubaliwa na miamba hiyo ya Uturuki.Tore,24,aliyefunga mabao sita na kutengeneza mengine manane wiki ijayo ataelekea England kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kusaini kuichezea Westham United.(FutbolArena)
Bennasser:AS Monaco imeendelea kukiimarisha kikosi chake tayari kwa msimu ujao wa Ligue 1 baada ya leo kumsajili kiungo, Youssef Aït Bennasser,19, toka Nancy kwa mkataba wa miaka mitano.(AS)
0 comments:
Post a Comment