Stevan Jovetic
Jovetic:Baada ya kuchemsha kumpata Mshambuliaji wa Leceister City Jamie Vardy,Arsenal imeripotiwa kumgeukia Mshambuliaji wa Inter Milan,Mmontenegro,Stevan Jovetic.Jovetic,26,mwenye uwezo wa kucheza kama mshambuliaji wa kwanza,wa pili, kiungo mshambuliaji na winga msimu uliopita aliifungia Inter Milan mabao sita katika michezo 26 ya Seria A.(Daily Mail)
Hamsik:Juventus imeripotiwa kutaka kutoa dau la €40m ili kuangalia uwezekano wa kumsajili kiungo wa Napoli, Mslovakia Marek Hamsik. Kwa mujibu wa wakala wake,Juraj Venglos,ni kuwa uwezekano wa Hamsik kubaki Napoli ni 50/50.(Tuttosport).
Promes:Arsenal imeendelea kuhusishwa wachezaji wengi tangu vuguvugu la usajili lianze na safari hii imehusishwa na mpango wa kutaka kumsajili winga wa Uholanzi na Spartak Moscow, Quincy Promes.(Mirror)
Zenga:Southampton imeendelea na harakati za kusaka Meneja mpya na sasa imeangukia kwa Kipa wa zamani wa Italia Walter Zenga.(Gazzetta dello)
Jesus:Manchester City imetuma ofa ya €21.5m (£16.7m) kwenda Palmeiras kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wake kinda, Gabriel Jesus lakini mpango huo huenda ukakwama hii ni baada ya Jesus,18, kuonyesha nia ya kutaka kujiunga na Barcelona.(One World Sports)
Valencia:Swansea City imehusishwa na kutaka kumsajili mshambuliaji wa West Ham United, Enner Valencia mwenye thamani ya £10m pamoja na mshambuliaji wa Liverpool Danny Ings mwenye thamani inayofanana na hiyo.(Daily Express)
De Gea:Rais wa Real Madrid,Florentino Perez rasmi ametanabaisha kuwa kwasasa klabu yake haina mpango wa kumsajili kipa wa Manchester United, David De Gea,24.(Daily
Express)
Dabo:Kiungo wa Montpellier Bryan Dabo amechagua kujiunga na Saint-Etienne licha ya kutakiwa na vilabu vingi vya nchini Uingereza.(L'Equipe)
Mori:Mkurugenzi wa Michezo wa Barcelona,Robert Fernandez alikuwa sehemu ya umati uliojitokeza kuutazama mchezo wa Robo Fainali wa Copa America kati ya Argentina na Venezuela lengo likiwa ni kumtazama kwa karibu beki wa Everton,Muargentina Funes Mori.(Sport)
Schneiderlin:Meneja mpya wa Everton,Mholanzi Ronald Koeman ameonyesha nia kutaka kafanya kazi mara nyingine na kiungo wake wa zamani Mfaransa Morgan Schneiderlin na tayari ameanza kuidodosa
Manchester United ili kuangalia uwezekano wa kumsajili.(People)
0 comments:
Post a Comment