Bejaia,Algeria.
MABINGWA wa soka wa Tanzania na wawakilishi pekee wa michuano ya kimataifa kwa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati,Yanga SC wameondoka mjini Bejaia,Algeria asubuhi ya leo kurejea Antalya,Uturuki kuendelea na kambi tayari kwa mchezo wake wa pili wa Kundi A wa kombe la shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo.
Yanga SC ambayo usiku wa kuamkia leo Jumatatu imeianza vibaya hatua ya makundi kwa kuchapwa na Mo Bejaia kwa bao 1-0 imeondoka ikiwa na kikosi chake kamili.
Ikiwa Antalya,Yanga SC itaendelea na mazoezi kama kawaida na inatarajiwa kurejea nyumbani wiki ijayo tayari kwa mchezo wake wa pili dhidi ya TP Mazembe utakaochezwa Juni 29,2016.
0 comments:
Post a Comment