Lille,Ufaransa.
UJERUMANI imefanikiwa kufuzu hatua ya Robo Fainali ya Michuano ya Ulaya (Euro 2016) baada ya Usiku wa leo kuifunga Slovakia kwa mabao 3-0 katika mchezo wa mtoano wa hatua ya 16 bora uliochezwa katika Uwanja wa Stade Pierre-Mauroy,Lille.
Mabao ya Ujerumani katika mchezo huo yametiwa kimiani na Jerome Boateng 8',Mario Gomez 43' na Julian Draxler 63'.
Kwa matokeo hayo Ujerumani sasa itacheza mchezo wake wa Robo Fainali kwa kuvaana na mshindi kati ya Italia ama Hispania.
VIKOSI
GER: Neuer; Kimmich, Boateng, Hummels,Hector; Khedira, Kroos; Ozil, Muller, Draxler;Gomez
SVK: Kozacik; Pekarik, Skrtel, Durica,
Gyomber; Skriniar, Kucka, Hrosovsky, Hamsik,Weiss; Duris
0 comments:
Post a Comment