Leceister,England.
MABINGWA Leicester City wameendelea kukiimarisha kikosi chao tayari kwa michuano ya Ligi Kuu England na ile ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao baada ya leo hii kumsajili beki wa kati wa Hispania, Luis Hernandez kwa uhamisho huru.
Hernandez,27,amesaini mkataba wa miaka minne wa kuwatumikia wakali hao wa King Power baada ya kumaliza kandarasi yake katika klabu ya Sporting Gijon inayoshiriki Ligi daraja la Kwanza Hispania maarufu kama La Liga.
Hernandez ni zao la shule ya soka ya klabu ya Real Madrid na aliwahi kuvichezea vikosi vyao vya timu B na C lakini mpaka Januari 2012 anajiunga na Sporting Gijon hakuwahi kuchezea kikosi cha wakubwa cha Real Madrid.
0 comments:
Post a Comment