London,England.
TOTTENHAM imemsajili Kiungo MKenya, Victor Wanyama toka Southampton kwa ada ya £11m.
Wanyama,24,amesaini kandarasi ya miaka mitano ya kuitumikia miamba hiyo ya White Hart Lane inayonolewa na Kocha wake wa zamani Southampton,Muargentina Mauricio Pochettino.
Akiwa na Southampton kwa kipindi cha misimu mitatu,Wanyama alifanikiwa kucheza jumla ya michezo 92 akipachika mabao manne na kuisaidia miamba hiyo ya St.Marys kumaliza katika nafasi za sita,saba na nane.
Wakati huohuo Celtic ambayo ni klabu ya zamani ya Kiungo huyo inatarajiwa kupata gawio la £1.1m kutoka katika usajili huo kutokana na kuwa na kipengele ya kupata gawio la asilimia 10 kutoka katika mauzo yoyote yatakayomuhusisha nahodha huyo wa Harambee Stars.
Wanyama alijiunga na Southampton mwaka 2013 akitokea Celtic kwa ada ya £12m.Msimu uliopita haukuwa mzuri sana kwake kwani alitolewa mara tatu dimbani baada ya kuonyeshwa kadi tatu nyekundu kwa mchezo mbaya.
0 comments:
Post a Comment