Mbeya,Tanzania.
MBEYA CITY imeendelea kukiimarisha kikosi chake tayari kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara hii ni baada ya kufanikiwa kumsajili Mshambuliaji, Mohammed Mkopi toka kwa mahasimu wao wa jiji la Mbeya,Tanzania Prisons.
Mkopi ambaye mwezi Februari mwaka huu alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi amesaini kandarasi ya mwaka mmoja kukitumikia kikosi hicho kinachonolewa na Mzambia,Khina Phiri.
Msimu uliopita Mkopi aliifungia Tanzania Prisons mabao sita Ligi Kuu Bara.Aking'aa katika michezo dhidi ya Mbeya City, Yanga, Mwadui na Mgambo Shooting ambapo alifunga bao moja na kupika mengine mawili na kuibuka kinara kwa mwezi Februari.
0 comments:
Post a Comment