728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, June 25, 2016

    EURO 2016:POLAND YAWA YA KWANZA KUFUZU ROBO FAINALI YAICHAPA USWISI KWA MATUTA


    Saint Etienne,Ufaransa.

    POLAND imekuwa timu ya Kwanza Kufuzu Robo Fainali ya Michuano ya Euro 2016 baada ya Jioni ya Leo kuifunga Uswisi kwa penati 5-4 Katika Mchezo mkali wa hatua ya 16 bora uliochezwa katika Uwanja wa Stade Geoffroy-Guichard,Saint Etienne.

    Mpaka dakika 120 za Mwamuzi Mark Clatternburg zinaisha matokeo yalikuwa sare ya bao 1-1.Poland ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza dakika ya 39 kupitia kwa Jacub BÅ‚aszczykowski.

    Dakika ya 82 Xhedan Shaqiri aliisawazishia bao Uswisi kwa tiki taka na kufanya mchezo uende mpaka dakika 120 ambazo nazo zilishindwa kumpata mshindi na mwamuzi kuamuru ipigwe mikwaju ya penati na Poland kuibuka washindi kwa penati 5 kwa 4.Granit Xhana alikosa penati kwa upande wa Uswisi.

    Kwa matokeo hayo Poland sasa itavaana katika robo Fainali na mshindi kati ya Croatia na Ureno siku ya Alhamis mjini Marseille


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: EURO 2016:POLAND YAWA YA KWANZA KUFUZU ROBO FAINALI YAICHAPA USWISI KWA MATUTA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top