Liverpool, England.
LIVERPOOL imekamilisha usajili wa Winga wa Senegal,Sadio Mane kutoka Southampton kwa ada ya £36m na atakuwa akivaa jezi namba 19.
Mane,24,amesaini mkataba wa miaka mitano wa kuitumikia miamba hiyo ya Anfield baada ya jana Jumatatu kufaulu vipimo vyake vya afya.
Mane ameiacha Southampton akiwa ameifungia mabao 21 katika michezo 67. Mane alijiunga na Southampton miaka mowili iliyopita kwa dau la £11.8m akitokea Red Bull Salzburg ya Austria.
0 comments:
Post a Comment