728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, June 21, 2016

    HIZI HAPA HABARI KUBWA ZA USAJILI TOKA BARANI ULAYA JUMANNE YA LEO JUNI 21,2016

    Lukaku.

    Lukaku:Arsenal imeripotiwa kuwa katika mazungumzo na Everton ili kuangalia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Ubelgiji,Romelu Lukaku,23, kwa kitita cha £31m.( TuttoMercatoWeb)

    Giggs:Ryan Giggs huenda akashindwa kuwa Meneja wa Nottingham Forest baada ya wamiliki wa klabu hiyo kuripotiwa kuwa na mpango wa kutaka kuajiri Meneja wa Kigeni.(Daily Mail)

    Remy:Meneja Mpya wa Chelsea, Antonio Conte, ameripotiwa kuwa amepanga kumpiga bei mshambuliaji wa klabu hiyo Mfaransa,Loic Remy,huku klabu ya Fenerbahce ikiripotiwa kuwa tayari kutoa £7m ili kumsajili staa huyo wa zamani wa Marseille na Queens Park Rangers.(Daily Express). 

    Townsend:Liverpool imekanusha kuwa ina mpango wa kutaka kumsajili winga wa Newcastle United,Andros Townsend,24, na badala yake imekiri kuwa na mpango wa wa kumsajili staa wa Southampton,Sadio Mane na winga wa Bayern Munich, Mario Gotze. (Liverpool Echo)

    Aucho:Meneja wa Aberdeen, Derek McInnes amethibitisha kuwa staa wa Uganda, Khalid Aucho atajiunga na klabu hiyo kwa majaribio ya muda mfupi na ikiwa atafaulu atasaini kandarasi ya kuichezea miamba hiyo ya Scotland.(Daily Mail)

    Nolito:Sergio Busquets na  Gerard Pique wameuomba uongozi wa klabu yao ya FC Barcelona kufanya kila uwezalo ili kumsajili Winga wa Celta Vigo Manuel Arago Nolito badala ya kuacha staa huyo wa Hispania atimkie Manchester City.( Manchester Evening News)

    Higuain:Gonzalo Higuain,28, hataweza kujiunga na Atletico Madrid msimu ujao hii ni kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Michezo wa Klabu hiyo Andrea Berta.(La Gazzetta dello Sport reports)
    .
    Deeney:Leicester City imeripotiwa kuandaa kitita cha £30m ili kujaribu kumsajili mshambuliaji wa Watford,Troy Deeney,hii ni baada ya kushuhudua ofa zake mbili za awali zikikataliwa.(The Sun)

    Ben Arfa:Hatem Ben Arfa,29, huenda akajiunga na Sevilla hii ni baada ya kuripotiwa kuwa katika mazungumzo ya mwisho mwisho ya kuhamia Ramon Sanchez Pizjuan.(L’Equipe)



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HIZI HAPA HABARI KUBWA ZA USAJILI TOKA BARANI ULAYA JUMANNE YA LEO JUNI 21,2016 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top