Southampton,England.
KLABU ya Southampton leo imemtangaza Mfaransa, Claude Puel kuwa Kocha wake Mkuu Mpya.
Puel ambaye hii ndiyo mara yake ya kwanza kufundisha soka nje ya Ufaransa, amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuinoa klabu hiyo ya St.Mary's akichukua nafasi ya Mholanzi,Ronald Koeman aliyetimkia Everton.
Kabla ya kutua Southampton,Puel,aliwahi kuvinoa vilabu vya Monaco,Lille,Lyon na Nice.Puel atakuwa akisaidiwa na Eric Black pamoja na Pascal Plancque kama makocha wasaidizi.
0 comments:
Post a Comment