Eduardo Sasha
Gameiro:Barcelona iko tayari kuketi meza moja na Sevilla ili kuanza mazungumzo ya kutaka kumsajili mshambuliaji Mfarasa,Kevin Gameiro.Barcelona imeamua kumgeukia Gameiro,27,baada ya kumkosa Manuel Arago "Nolito" anayeelekea Manchester City.Mpango huo wa Barcelona huenda ukawa mgumu kwani Sevilla imeripotiwa kuwa haitakuwa tayari kumwachia staa huyo kwa dau la chini ya €40m (£30.7m).(AS)
Sasha:Leicester City imefanikiwa kuizidi kete Arsenal na kumbakisha mshambuliaji wake,Jamie Vardy lakini huenda ikashindwa kumsajili mshambuliaji wa Kibrazil, Eduardo Sasha baada ya ofa yake ya €9m kukataliwa na klabu yake ya Internacional.Internacional inataka €12m ili iweze kumuachia Sasha,22.(Globoesporte)
Ramsey:Meneja wa Manchester United,Jose Mourinho ameripotiwa kuwa atatoa ofa ya £50 ili kumsajili kiungo wa Arsenal Aaron Ramsey,24, ikiwa atashindwa kumsajili kiungo wa Borussia Dortmund, Henrikh
Mkhitaryan,27.(The Sun)
Nani:Vilabu vya Liverpool na Everton vimeingia katika vita ya kumtaka winga wa Fenerbahce, Luis Nani,27,lakini vinakabiliwa na upinzani mkali toka kwa vilabu vya Inter Milan na Valencia ambavyo vimeonyesha nia ya kumtaka staa huyo wa zamani wa Manchester United.(gianlucadimarzio)
Rodgers:Meneja Mpya wa Celtic, Brendan Rodgers ameshindwa kukanusha ama kukubali habari ziliozoenea kuwa anataka kumsajili kiungo wa Liverpool, Joe Allen,26.(South Wales Evening Post)
Allen:Liverpool imekataa ofa ya £8m toka Swansea City kwa ajili ya kumuuza kiungo wake Joe Allen.Taarifa zaidi zinasema Liverpool itakuwa tayari kumuuza Allen,26,ikiwa Swansea City itakuwa tayari kutoa £10m.(The Mirror)
Sturaro:Vilabu vya Crystal Palace na Chelsea vimeripotiwa kuonyesha nia ya kutaka kumsajili kiungo wa Juventus, Stefano Sturaro.Msimu uliopita Sturaro,23,aliichezea Juventus michezo 19 katika Ligi ya Seria A.
Zielinski:Staa wa Udinese, Piotr Zielinski,23,hatasaini kuichezea Liverpool Mpaka hapo Poland itakapokuwa imehitimisha ushiriki wake katika michuano ya Euro.Udinese imedaiwa kukubali dau la £12m kutoka Liverpool.(Liverpool Echo)
0 comments:
Post a Comment