Turin,Italia.
RASMI Klabu ya Juventus imemsajili mlinzi wa kulia wa Brazil, Dani Alves kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kufaulu vipimo vyake vya afya.
Alves,33,ametua Juventus baada ya kuomba kuondoka Barcelona licha ya kwamba alikuwa amebakiza miezi 12 katika mkataba wake.
Alves anakuwa mchezaji wa pili kujiunga na Juventus baada ya kiungo wa Bosnia,Miralem Pjanic aliyetua Turin akitokea AS Roma kwa ada ya £30m.
Akiwa na Barcelona,Alves aliweza kuisaidia klabu hiyo ya Catalunya kutwaa vikombe 23 katika kipindi cha miaka minane alichohudumu Nou Camp akitokea Sevilla mwaka 2008 kwa ada ya €30m.kkll
0 comments:
Post a Comment