728x90 AdSpace

Sunday, June 26, 2016

SASA KUZIONA YANGA,TP MAZEMBE SHIRIKISHO BURE KABISA,VIINGILIO VYAFUTWA

Dar es Salaam,Tanzania.

UONGOZI wa Yanga SC umefuta viingilio vyote ilivyopanga vitumike katika Mchezo wake wa Kombe la Shirikisho siku ya Jumanne dhidi ya TP Mazembe ya DRC na sasa Mashabiki wataingia Bure Kabisa.

Yanga SC imesema lengo la kufuta viingilio vya awali vya Tsh 7,000 kwa Jukwaa la Mzunguko na Tsh 30,000 kwa VIP ni kuhakikisha WATANZANIA na Wapenda Kandanda wote wanapata nafasi ya kuushuhudia Mchezo huo unaotarajiwa kuwa utakuwa wa kukata na shoka.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: SASA KUZIONA YANGA,TP MAZEMBE SHIRIKISHO BURE KABISA,VIINGILIO VYAFUTWA Rating: 5 Reviewed By: Unknown