728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, June 22, 2016

    EURO 2016:CROATIA YAICHAPA HISPANIA NA KUONGOZA KUNDI D,16 BORA SASA NI ITALIA NA HISPANIA

    Bordeaux,Ufaransa.

    BAO la dakika za mwisho la winga, Ivan Perisic limeipeleka Croatia kileleni mwa Kundi D na kuifanya ifuzu hatua ya 16 bora ya michuano ya Euro 2016 baada ya Jumanne usiku kuichapa Hispania kwa mabao 2-1 katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Matmut Atlantique huko Bordeaux.

    Hispania ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza baada ya Alvaro Morata kufunga dakika ya 7 ya kipindi cha kwanza akimalizia pasi ya Cesc Fabregas.



    Dakika ya 45 Nikola Kalinić aliisawazishia bao Croatia kabla ya Ivan Perisic kufunga bao la ushindi dakika ya 87 na kuipeleka hadi kileleni mwa Kundi D.

    Pia katika mchezo huo Sergio Ramos aliikosesha Hispania nafasi ya kuambulia japo sare baada ya mkwaju wake wa penati kudakwa na kipa wa Croatia, Danijel Subašić.

    Kwa matokeo hayo Hispania itavaana na Italia katika hatua ya 16 bora.

    Katika mchezo mwingine wa kundi D Uturuki imefufua matumaini ya kufuzu hatua ya 16 bora baada ya kuifunga Czech kwa mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa huko Stade Felix Bollaert-Delelis .

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: EURO 2016:CROATIA YAICHAPA HISPANIA NA KUONGOZA KUNDI D,16 BORA SASA NI ITALIA NA HISPANIA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top