728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, June 29, 2016

    BORA YANGA,AL AHLY NDIVYO HOVYO KABISA YAENDELEA KUGAWA POINTI LIGI YA MABINGWA AFRIKA

    Alexandria, Misri.

    WAKATI Yanga SC ikionekana kupoteana katika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho Afrika kwa kupoteza michezo yake miwili ya awali ya kundi A,Vigogo wa soka la Misri Al Ahly ndiyo wameendelea kuonekana hovyo zaidi katika hatua kama hiyo lakini katika mashindano ya klabu bingwa Afrika baada ya Jumanne usiku wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Borg El Arab Stadium ulioko Alexandria kukubali kichapo cha mabao 2-1 toka kwa ASEC Mimosas ya Ivory Coast.

    Baada ya kupoteza mchezo wake wa kwanza kwa kufungwa mabao 3-2 na Zesco United huko Ndola,Zambia, ilitegemewa Al Ahly wangeamka na kuutumia vyema uwanja wao wa nyumbani lakini kinyume na matarajio ya wengi wamekubali kichapo kwa mara ya pili mfululizo na kujikuta wakishuka mpaka mkiani mwa msimamo wa kundi A lenye timu za Wydad Casablanca,Zesco United na ASEC Mimosas.

    Wageni ASEC Mimosas waliokuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza baada ya Yannick Krahire Zakri kufunga dakika ya 29' kwa mkwaju mkali kabla ya Armand Niamke kufunga la pili dakika ya 80'.Bao la wenyeji Al Ahly limefungwa na Ahmed Hegazy dakika ya 53'.

    Mchezo mwingine wa kundi hilo utaendelea tena leo Jumatano kwa Wydad Casablanca ya Morocco kuwa mwenyeji wa Zesco United ya Zambia.Timu zote mbili zina pointi tatu baada ya kushinda michezo yao ya awali dhidi ya ASEC Mimosas na Al Ahly.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BORA YANGA,AL AHLY NDIVYO HOVYO KABISA YAENDELEA KUGAWA POINTI LIGI YA MABINGWA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top