Lyon,Ufaransa.
UFARANSA imefanikiwa kufuzu hatua ya Robo Fainali ya Michuano ya Euro 2016 baada ya jioni ya Leo kutoka nyuma na Kuifunga Jamhuri ya Ireland kwa mabao 2-1 katika mchezo mkali wa hatua ya 16 bora uliochezwa katika uwanja wa Stade de Lyon,Lyon.
Shujaa katika mchezo wa leo alikuwa ni mshambuliaji Antoine Griezmann aliyeifungia Ufaransa mabao yote mawili dakika za 58 na 61.Bao la Jamhuri ya Ireland limefungwa dakika ya 2 kwa mkwaju wa penati na Robbie Brady.
Mkwaju huo wa penati ulipatikana baada ya Paul Pogba kumwangua Shane Long ndani ya eneo la penati.
0 comments:
Post a Comment